Historia fupi ya Zahanati Background


Zahanati ya EAGT Utemini ilianzishwa mnamo mwishoni mwa mwaka 2010, inamilikiwa na kanisa la EAGT UTEMINI, ilianzishwa na Kanisa la EAGT Utemini ili kutoa huduma bora za afya kwa watu wote. Tulianza huduma zetu katika nyumba ya kukodi, tukitoa Huduma za Nje (OPD) zinazojumuisha ushauri wa daktari, uchunguzi wa maabara kwa vipimo vya msingi na Dawa, lakini baadaye mnamo mwaka wa 2012 tulihamia kwenye jengo letu wenyewe. Kukamilika kwa jengo letu tuliweza kupanua Zahanati kufikia sasa tunatoa huduma za matibabu ya jumla, afya ya mama na mtoto na kliniki maalumu. Mpango wetu wa baadaye ni kuboresha na kufikia ngazi ya hospitali, kuongeza majengo na kuongeza huduma nyingine maalumu.
Mashirika tunayo fanyanayo kazi.

  • MURIGHA GIRLS
  • ST. CENTER (UNYIANGA, FPCT Kibaoni, EAGT BEROYA)
  • CRDB pre paid card, VISA,MASTER Card

MAONO/MWELEKEO.


Mwelekeo wetu ni kufikia viwango vya hali ya juu katika utoaji wa huduma za afya na kuweka wagonjwa Na familia zao kwanza, kwa msaada wa Mungu mponyaji mkuu.

DHAMIRA


Kuboresha afya zawagonjwa na jamii kwakutoa huduma zinazo zingatia ubunifu, huruma, ujuzi, maarifa na teknolojia kwaneema tuliyopewana Mungu.