Huduma zetu zimegawanywa katika sehemu zifuatazo:

  • • Idara ya wagonjwa wa nje (OPD) na ushauri.
  • • Vipimo.
  • • Dawa.
  • • Kliniki Maalum.
  • • Kliniki ya afya ya uzazi na mtoto (RCH).
  • • Maombi na maombezi.


Wagonjwa wa nje (OPD) na ushauri

Idara ya Wagonjwa wa nje(OPD) hutoa huduma za kimatibabu na upasuaji mdogo kwa wagonjwa wa rikazote na kupumzisha. Lengo letu ni kutoa huduma bora za kimatibabu sambamba na uchunguzi wakimaabara wa kisasa,tukifanya huduma kwa mgonjwa kuwa huduma nzuri na rafiki iwezekanavyo. Idara hii ina vyumba vitatu vya ushauri wa kitaalam. Katika idara hii wahudumu wetu hu-udumia takriban wagonjwa 4,000 kila mwezi. Tunashirikiana kwa karibu sana na idara nyingine zote katika zahanati


Vipimo. Uchunguzi wa kimaabara

Zahanati ya EAGT utemini inatoa vipimo vya msingi vya maabara zinazo jumuisha vipimo vya vimelea(parasitology) na mikrobiolojia(microbiology) ambayo dhamana ya ombi iliyoagizwa na madaktari inaweza kufanyika. Idara inafanya kazi karibu saana ili kutoa huduma za utafili na ubora wa hali ya juu ili kusaidia katika huduma nzuri ya mgonjwa. Kwa wastani idara inahusika na sampuli tofauti ambazo ni pamoja na, damu, mkojo na kinyesi. Inahudumia wagonjwa takriban 2700 kila mwezi. Maabara hufanya kazi kwa karibu na idara zote na kliniki ndani ya hospitali.


DUKA LA DAWA.

kwa ushirikiano wa karibu na idara nyingine, wagonjwa watakaohitaji dawa hupata dawa hizo hapa(duka la dawa) hii ikijumuisha dawa za msingi(tracer medicine), dawa za msingi zote katika kiwango cha zahanati, dawa za ugonjwa wa sukari, shinikizo la damu na dawa zingine mbalimbali. tunatoa huduma rafiki na kwa wakati, kwa kuwa mgonjwa anahitaji kuelewa vizuri maelekezo ya namna ya kutumia dawa aliyo andikiwa. Mara nyingine tuna hudumia na wagonjwa waliokosa dawa katika maduka mbalimabali ya dawa hapa mjini, wakitoka hospitali mbalimbali za hapa mjini, hupewa dawa endapo watakuwa na formu ya dawa(prescription) kutoka katika kituo cha afya kinachotambulika au baada ya kuonana na madaktari wetu. Malengo yetu ni kutoa kuhuduma za kisasa zaidi kwa wagonjwa wote.


KLINIKI MAALUM.

  • Kisukari na Shinikizo la Damu.

    Kisukari ni moja ya sababu zinazoweza leteleza shinikizo la damu. Hata hivyo inawezekana kuwa na shinikizo la damu kwa miaka mingi bila kuwa na dalili yeyote. Ushauri wa ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu katika EAGT Utemini hutoa ujuzi bora wa maeneo hayo. Tunasaidia wagonjwa kupunguza shinikizo la damu na wagonjwa ambao wana shinikizo la damu ambayo si rahisi kudhibitiwa. Endapo itahitajika tunasaidia matibabu pia, mara nyingi tunasaidia wagonjwa kufikia shinikizo la damu la chini kwa dawa chache iwezekanavyo. Tunasaidia wagonjwa kutambua chakula na mazoezi ambayo inaweza kusaidia kupunguza shinikizo la damu na kuboresha ngazi za kiafya. Tunaangalia hali nyingine zinazoathiri afya zao mfano ugonjwa wa kisukari. Kwa njia ya kufuatilia mara kwa mara, tunafanya matibabu kwa matokeo bora na dawa kidogo, tunahudumia takribani wagonjwa 144 kwa jumla ya mahudhurio manne yanayopangwa kila jumamosi ya kila mwezi na hivyo kila mteja huwa na hudhurio moja kila mwezi.

  • Kliniki ya afya ya uzazi na mtoto.

    Kliniki ya afya ya uzazi na mtoto (EAGT RCH).iliyofunguliwa mwishoni mwa mwaka wa 2016. Sasa inajulikana kwa kutoa huduma ya clinic, hivyo zahanati ya EAGT Utemini imejitolea kusaidia kupunguza takwimu mbaya za nchi juu ya vifo vya uzazi na watoto Na maradhi kama ilivyo sasa nchini kwa mwaka (chanzo: WHO): vifo vya uzazi, 13,000; Vifo vya watoto wachanga, 45,000; Na vifo kati ya watoto chini ya umri wa miaka mitano, 157,000. Changamoto zinazoendelea dhidi ya kupunguza vifo vya mama / mtoto ni: ukosefu wa miundombinu, umasikini, magonjwa na uhaba wa wafanyakazi na huduma za matibabu.

  • Kliniki ya Meno.

    Huduma za EAGT Utemini dispensary zinazidi kuwa karibu na rafiki zaidi kwa wagonjwa na familia zao. Tumeanza kliniki maalumu kwa ajili ya huduma za matibabu ya kinywa na meno kwa kutoa huduma zifuatazo

    • • Kung’oa meno.
    • • Kusafisha meno.
    • • Kuziba meno
    • • Kubadili meno rangi (veneering ).
    • • Kufunga mataya yaliyo vunjika .
    • • Kurekebisha meno yaliyo katika mpangilio mbaya.
    • • Kutengeneza meno bandia .
    NB:HUDUMA YA X-RAY YA MENO ITAFANYIKA.


Maombi na Maombezi.

Zahanati ya EAGT Utemini hufanya kazi chini ya kauli mbiu inayotuongoza kwamba "Tunatibu Mungu Anaponya" - kutambua umuhimu mkubwa wa Mungu katika uponyaji wa kiroho na wa kimwili wa wagonjwa wetu na familia zao. Ingawa wafanyakazi wote wa zahanati ya EAGT Utemini wanashuhudia kipengele cha kiroho cha utume huu wote, watumishi wa EAGT Utemini huongoza kazi hii muhimu sana. Inapatikana kwa wagonjwa na wateja wote kwa saa 24 siku saba za wiki.Wahudumu wetu u-hubiri na kutoa faraja ya kiroho, sala na maombezi ya huruma hutolewa karibu na mgonjwa. Msaada wa kisaikolojia kwa wagonjwa ambao wanaweza kuhitaji msaada huo nayo inapatikana. Wahudumu wetu hu-hudumu tu kwa wagonjwa, lakini hukaa pamoja na familia za wagonjwa pia, wakati wote wa furaha na huzuni.